Ambwene Mwasongwe presents the Official Music Video For "Picha Ya Pili"
Stream/Download: orcd.co/pichay...
PICHA YA PILI
Ni wimbo unaokutaka uanze kuiona picha ambayo huwezi kuiona kikawaida, Picha hii wengi wetu hatunayo, na kwa kuikosa tumefanya maamuzi mengi bila kufikiria na kwa sababu hiyo tumeongeza maumivu makali kwa wenzetu hasa wenye hali tofauti na sisi.
Mwanadamu ni kiumbe mwenye akili na mara zote amekuwa akijitahidi sana kuficha hali yake halisi ya maisha, ndio maana akitoka nyumbani, huoga, hupaka mafuta, hutabasamu, na ukimuangalia na kumsikia kwa picha ya kwanza unaweza danganyika ukadhani kafanikiwa sana, ana furaha, kapendeza na mambo yake ni mazuri.
Lakini akibaki peke yake mahali hakuna mtu anamuona hali yake halisi huwa wazi na hana cha kuficha, huko hulia sana, huugua sana, hulalamika sana, na huko ndiko anakosononeka na kupata vidonda vya tumbo, sukari, presha na msongo wa mawazo. Huko huchakata kila neno, kila tendo, kila lugha ya mwili uliyomwonyesha na hutengeneza maana ya kila tukio.
Hivyo kila unapokutana naye na kutenda jambo lolote mfikirie kwa picha hii ya pili, na jaribu kuvaa viatu vyake kwamba ungekuwa wewe ungepokeaje maneno, matendo, zawadi, na tukio ambalo wewe umefanya kwa mwenzako.
UNAWEZA toa zawadi kwa yatima, wajane, maskini, vichaa, walemavu ukafurahi ukadhani umefanya jambo jema sana,( ni kweli umefanya vyema) Lakini je! umeitafakari njia uliyotumia kutenda hayo? je! ingetumika kwako ungefurahi? au nawe ungeenda mahali pa peke yako na kulia, kuugua na kusononeka?
Jaribu kufikiri umepoteza mume wako, au wazazi wako, au kiungo chako cha mwili, Au hali yako ya maisha, kisha wanakusaidia watu kwa michango na fedha, nguo, chakula nk lakini wanakusimamisha mbele ya kadamnasi au kamera kukupa na wanakupost kila mtu aone uyatima wako, ujane, hali yako, ulemavu wako! Unahisi ukikaa peke yako utaona muujiza, fahari, bahati au utaona wametonesha kidonda cha maumivu? maana hukupenda kuwa na hali hiyo, hivyo msaada ni matokeo ya hali yako, ukiwasilishwa vibaya hauwi baraka unakuwa maumivu.
NINAKUSIHI KWA HURUMA YA YESU KRISTO UPOKEE WIMBO HUU, CHUKUA HATUA KWA AJILI YA MUNGU WASAIDIE WASIOJIWEZA, YATIMA, WAJANE, WALEMAVU NA MASKINI BILA KAMERA, MATANGAZO, NA USHABIKI MAANA HUJUI KESHO ITATOKEA KWA NANI.
Unafanya vyema kusaidia ila fanya vizuri zaidi kwa kuzingatia heshima ya unayempa kama mtu wa Mungu na wewe kama unampa Mungu.
Watch All Music Videos by Ambwene Mwasongwe: • Ambwene Mwasongwe All ...
Follow Ambwene Mwasongwe
Instagram: / ambwenemwasongwe_
Subscribe to Ambwene: / @ambweneobadiamwasongwe
Digital Branding & Marketing By:
Black Ozen Entertainment Limited: / blackozenentertainment...
JICHO LA PILI (lyrics)
Verse 1
Yahitaji macho ya moyo, kuona picha ya pili.
Yahitaji sikio la ndani, kusikia sauti ya moyo.
Nimeona chozi likitiririka, kwenye uso unaocheka.
Nimesikia sauti ya kuugua, katikati ya kigelegele.
Nimeona watu wakienda, kuwaona wahitaji, ila wamebeba kamera uuuh! kuuonyesha ulimwengu.
Yatima nao wajane, mbele ya kamera, hushukuru kwa kutabasamu.
Ila wakibaki peke yao na Mungu hulia kwa kuugua.
Sababu ya uyatima, sababu ya ujane, ni kama twadhalilishwa,. HAWAJUI size ya kiatu hiki namna kinavyobana, Hawajui twaumia.
Chorus 1
Ni Yesu tu, Ni Yesu, Anayeletaga faraja ya moyo kwa aliyeumizwa na kuvunjwa vunjwa bila matangazo... (wewe Yesu u mwema kwetu yooh!..)
Ni Yesu tu ,ni Yesu anayetoaga neno la faraja la moyo, liwe hadharani au la sirini wala haliumizi.
(Ni wewe ufanyaje kwa kutufikiria utu wetu)
Ni yesuuu tu ni Yesu anayetoaga Neno la Faraja Liwe hadharani au la sirini wala Haliumizi
Verse 2
Nilimwona mama analia, mtoto wake kawa teja, anavuja mate mtaani, wenzake wanamcheka.
Wanapiga picha naye wanafanya self wanapost wanacheka.
Wanainjoi wanatafuta views hawajui maumivu ya mzazi.
Kicha kwa mwenzako anachekesha sana, akiwa kwako anauma.
Mlemavu kwa jirani anaburudisha, akiwa kwako anauma.
Niliona wazazi wanalia eeeh! malezi yamewashinda, wamejitahidi sana kusema, watoto hawasikii.
Wanasikia mtaani wanasemwa vibaya, bado hawakati tamaa.
Hata kama ni mwizi, hata kama malaya, ni mtoto wangu hakati tamaa.
Chorus 2
Ni Yesu tu, Ni Yesu asiyewatupa tusiowajali, tunaowasema tuliowachoka na kuwadharau. (eeheee)
Ni Yesu tu Ni Yesu anayeletaga jibu la maswali kwa waliochoka, wenye utata na waliokwama (eeeheee!)
Ni Yesu tu Ni Yesu anayeletaga jibu la maisha kwa waliochoka, wenye maswali, na wenye utata. (Bwana nakuombaaa)
Verse 3
Naomba wakumbuke, tuliowachoka, tunaowasema, tunaowadharau. Bwana warehemu ni watoto na utusamehe.
Samehe makosa Yetu samehe raha yetu, tumefurahiii tukadhani tumefanya kwa ajili yao kumbe kwa ajili yetu.
Samehe Bwana kuwatangaza wao bila kujali utu.
Ni Yesuuuu Ni Yesuuu Ni Yesuuu oooh! Ni Yesuuuu Ni Yesuuu, Ni Yesuuuu, Ni Yesuuuu uuu
#AmbweneMwasongwe #PichaYaPili
Негізгі бет Ambwene Mwasongwe - Picha ya Pili (Official Music Video)
Пікірлер: 939