Mbunge wa Konde (ACT Wazalendo), Mohamed Said Issa ameitaka Serikali kurejesha upya utaratibu wa watu wote wanaoingia Zanzibar kuwa na hati ya kusafiria.
Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Makamu wa Rais kwa mwaka 2024/25 leo Jumanne Aprili 24,2024, Issa amesema lengo ni kuvilinda visiwa hivyo.
“Kwa nini waliweka pasipoti (hati za kusafiria) visiwa vile vinahitaji kulindwa, mimi sikubaliani na suala la kutovilinda visiwa saa hizi. Sasa hivi Zanzibar imejaa watu na tunavyoendelea hawatakuwa na sehemu ya kuishi,”amesema.
Issa amempongeza, hayati Abeid Karume kwa kujenga maghorofa yale (hakusema yako wapi) kwa kuwa alitaka Wazanzibar wote wakae humo, kwa sababu aliona ardhi ni ndogo sana.
“Sasa hivi ukienda pale Zanzibar utakuta viwanja vimechukuliwa, miti imekatwa, kulikuwa na zao la mikarafuu haliko tena, imebakia Pemba tu na kule Pemba linakwenda kuisha minazi hakuna sasa hivi tunaagiza kutoka Mafia ,”amesema.
Amesema jambo hilo sio zuri na hata ajira za watalii hawapati tena Wazanzibar wanaofanya kazi hizo ni wageni.
Негізгі бет Dakika 8 za Mbunge aliyetaka kuingia Zanzibar kutoka Tanzania bara iwe kwa pasipoti
Пікірлер: 95