Mjadala mkali umeibuka Bungeni leo Juni 03,2024, kufuatia Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka kuuliza msimamo wa serikali kuhusu nyaraka iliyovuja inayoonesha mapendekezo ya kubadili maeneo ya wafugaji Kaskazini kuwa mapori tengefu.
Nyaraka hiyo imeendelea kuzua gumzo kubwa katika jamii za wafugaji hasa kutokana na sehemu kubwa ya Ardhi inayopendekezwa kufanywa hifadhi.
Akijibu hoja ya Ole Sendeka Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki alieleza kuwa suala hilo sio rasmi.
"Nyaraka hiyo ambayo anaitaja haipo mezani kwangu, haijatolewa na chombo rasmi kwa hiyo nilikua naomba wala tusiizungumzie kwa sababu tunazidi kuleta taharuki kwa wananchi. Mheshimiwa Spika taratibu za kiserikali zinajulikana,namna ya kutenga maeneo kama mapori tengefu zinajulikana, kama itafika wakati huo na tathmini hiyo itakuwa inaendelea basi taratibu za kiserikali rasmi zitafanya kazi," alieleza Kairuki
Hata hivyo Ole Sendeka alionesha kutokuridhika na kutaka majibu Zaidi kutoka serikalini.
"Namheshimu sana Waziri, lakini wa kweli Mheshimiwa Waziri kwanza niseme sipokei taarifa na sipokei kwa sababu moja, mchakato ulipoanza ulianzia Bungeni kufuatia taarifa ya Waziri katika bajeti ya 2021/22 ya kupandisha hadhi mapori hayo, wakaenda kutuma timu za wataalamu zimekuja katika Wilaya zetu," alieleza Ole Sendeka.
"Watalamu Wameleta taarifa, bahati mbaya taarifa yao ilipoletwa kwa Waziri ikavuja na taarifa hiyo ni hii hapa. Taarifa hiyo wananchi wote wanayo, tukijifanya hatuioni inatuharibia kura katika ukanda wa Kaskazini. Kwa sababu taarifa wananchi wanayo na bahati mbaya taarifa sio nzuri inapendekeza maeneo karibu yote ya wafugaji katika wilaya hizo zibadilishwe ziwe mapori tengefu,"
Mjadala uliendelea huku Ole Sendeka akiitaka serikali iikatae taarifa hiyo, jambo ambalo halikufanyika.
Негізгі бет Serikali Yashindwa Kuikataa au Kuikubali Taarifa Yake.Ni Kuhusu Kuongeza Maeneo ya Hifadhi Kaskazini
Пікірлер: 40