Siku moja baada ya Tumsime Ngemela kutoka hadharani akiziomba mamlaka za haki kumfikisha mahakamani aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahya Nawanda akidai alimlawiti, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amesema anaviachia vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza tuhuma za yeye kuhusika kwenye sakata hilo.
Akizungumza jana na waandishi wa habari, Tumsime ambaye ni mwanafunzi wa chuo kimoja jijini Mwanza, amedai baada ya tukio la kulawitiwa lililotokea Juni 2, 2024 lililotokea kwenye gari dogo alilodai ni la Dk Nawanda, alitoa taarifa polisi.
Hata hivyo, amesema kiongozi mmoja mkoani Mwanza alimtaka kufuta kesi hiyo ili suala hilo limalizwe kifamilia.
Kufuatia madai hayo, Mtanda ameibuka leo Jumamosi Julai 6, 2024 kwenye hafla ya kutoa zawadi kwa wakaguzi na askari polisi waliofanya vizuri mwaka 2024, akidai amekuwa mvumilivu baada ya kusikia watu wakimsema vibaya mtandaoni.
Huku, akiitaja falsafa ya Rais ya 4R, Mtanda amesema kwa kuwa yeye ni mstahimilivu wa kisiasa hana haja ya kumjibu kila mtu, kwa kuwa anajua tayari vyombo vya usalama vinafanya kazi yake, huku akitaka viachwe vitimize wajibu wake bila kuingiliwa.
Негізгі бет Mtanda ataka haki sakata la kutajwa kumkingia kifua Dk Nawanda
Пікірлер: 34